NA EBEN-EZERY MENDE
SHIRIKISHO la Michezo ya Pentathlon Tanzania (PMT) limeshiriki utaratibu wa kufanya usafi katika Fukwe za Dengu jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na wanamichezo na washiriki waliokutana kwenye fukwe hizo kwa ajili ya kushiriki kufanya usafi Mkurugenzi wa Ufundi wa mbio za vikwazo, Bw. Joshua Kayombo (Joka) amesema utaratibu huo umezinduliwa leo Aprili 5,2025 na utakuwa endelevu.
Kayombo amesema mchezo wa mbio za vikwazo unatakiwa kufanyika maeneo safi na salama na eneo la fukwe nalo ni miongoni mwa maeneo ya kufanyika michezo hiyo hivyo ni lazima yawekwe katika hali ya usafi.
"Michezo ya Mbizo za vikwazo huzingatia mambo mengi na miongoni ni sehemu safi na salama kwa mshiriki. Fukwe tutakazotumia kwa michezo hiyo lazima tuhakikishe ziko katika hali hiyo," amesema Kayombo.
Amesisitiza kwamba michezo ni afya kwa kila binadamu hivyo ni jambo la kuzingatiwa ili kuepuka maradhi yasiyo ambukiza.