ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewapongeza wachezaji wa timu ya Simba kwa ushindi walioupata katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, katika mchezo wa awali wa Nusu Fainali dhidi ya timu ya Stellenbosch Football Club ya Afrika Kusini.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza timu ya Simba kwa kuuchagua Uwanja wa New Amaan Complex kuwa uwanja wao wa nyumbani na kueleza kuwa Serikali imefarijika na hatua hiyo, huku akiahidi kuendelea kuimarisha viwanja mbalimbali hapa Zanzibar.