Rais Dkt.Mwinyi akutana na Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza,Tony Blair

LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tony Blair Institute for Global Change (TBI), Sir Tony Blair kwa ushirikiano wake katika sekta mbalimbali ikiwemo kuimarish bandari, utalii na kuwajengea uwezo Taasisi ya Ufuatiliaji na Usimamizi wa Serikalini (PDB).
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo Aprili 6,2025 alipozungumza na Waziri Mkuu Mstaafu huyo, alipomtembelea kwenye makazi yake The South Pavillion, Cotton Underwood Aylesbury, Uingereza.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemhakikishia kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu katika kuendeleza Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Naye Waziri Mkuu mstaafu Tony Blair amemuahidi Rais Dkt.Mwinyi kuendelea kushirikiana na Zanzibar katika uchumi wa kidigitali,utalii,uwekezaji kupitia taasisi yake ya TBI.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Dkt.Saada Mkuya, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe.Mbelwa Kairuki, Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post