ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi katika maziko ya mwandishi wa habari mwandamizi marehemu Hassan Abdalla Khamis aliyefariki jana.
Rais Dkt.Mwinyi alishiriki katika sala ya kusalia maiti Msikiti wa Al AZHAR Magomeni Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.
Aidha,Dkt.Mwinyi alifika nyumbani kwa marehemu Mpendae kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa na kuwataka kuwa na subira wakati huu wa msiba huo mzito.

Marehemu amezikwa kijijini kwao Muyuni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.