Rais Dkt.Mwinyi awakaribisha wafanyabiashara wa Uingereza kuwekeza Zanzibar

LONDON-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka Uingereza kuwekeza Zanzibar katika fursa mbalimbali ikiwemo sekta ya Uchumi wa buluu, utalii, usafiri wa baharini, uvuvi,nishati na miundombinu ya kidijitali.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipojumuika kwenye chakula cha jioni na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za biashara na uchumi za Uingereza kilichoandaliwa na Taasisi ya Eastern Africa Association ya Uingereza katika Jiji la London, tarehe 7 Aprili 2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema katika kipindi cha Miaka 4 Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua zaidi ya asilimia 7 kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta mbalimbali.Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa wawekezaji hao kuwekeza katika zao la Mwani, ameeleza kuwa Zanzibar ndio mzalishaji namba moja wa zao hilo Afrika ambalo soko lake linaendelea kukua zaidi.

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post