ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatembelea wagonjwa na kuwafariji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Lumumba, leo Aprili 1,2025.
Wagonjwa waliotembelewa ni Bi.Arafa Mohamed Said na Kanali mstaafu mzee Masoud Khamis Juma.
Rais Dkt.Mwinyi amewatakia heri na kuwaombea kupona haraka. Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amekuwa na utaratibu wa kuwafariji wagonjwa.