DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa taasisi za umma, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Prof. Emanue Mjema ameteuliwa kuendelea na kipindi cha pili kama Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mhandisi Mwanasha Tumbo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), akichukua nafasi ya Prof. Esnat Chaggu aliyemaliza muda wake.
IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo.
Rosemary Silaa ameteuliwa kuendelea na kipindi cha pili kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD).