Rais Dkt.Samia atunuku Nishani za Kumbukumbu ya Muungano kwa viongozi mbalimbali

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kuendelea kuuenzi Muungano kwa kutoruhusu migogoro itakayochelewesha maendeleo nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya kutunuku Nishani za Kumbukumbu ya Muungano kwa viongozi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais Samia amesema hayo leo Aprili 26, 2025 mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kutunuku Nishani ya kumbukumbu ya Muungano iliyoenda sambamba na uzinduzi wa kitabu cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Ali Shein kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwa Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwakilishi wa Familia ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwa Spika Mstaafu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili kwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Nne Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Pili Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwakilishi wa Familia ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Balozi Mhandisi John William Kijazi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.

Sambamba na hilo wakati akizungumzia uzinduzi wa kitabu, Rais Samia amesema kuwa Hayati Baba wa Taifa alionesha mapenzi makubwa kwa wanawake wa Kitanzania kwa kuhakikisha wanapata nafasi katika uongozi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya Muungano Daraja la Tatu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara (2012-2022) Mhe. Philip Japhet Mangula kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 26 Aprili, 2025.

Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaasa vijana kukisoma kitabu hicho ili kuenzi maandiko ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news