Rais Kiir,Museveni wajadili mambo muhimu

JUBA-Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wamejadiliana umuhimu wa kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.
Aidha, viongozi hao wawili katika mazungumzo yao ya Aprili 3,2025 yaliyofanyika mjini Juba, walijadili kuhusu hali ya kisiasa na usalama nchini Sudan Kusini na ukanda wote wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini, Ramadan Mohammed Abdallah Goc amesema, mkutano huo umelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Juba na Kampala katika sekta mbalimbali.

Pia, amesema mkutano huo uliangazia hali ya usalama nchini Sudan Kusini.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda nchini Uganda, John Mulimba amesema, mkutano huo uliangazia masuala ya amani na usalama katika nataifa hayo mawili na ukanda wote kwa ujumla.

Aidha, maafisa waandamizi walidokeza kuwa, mazungumzo ya marais hao yanatarajiwa kuleta matokeo chanya katika kuimarisha umoja, ustahimilivu na mshikamano katika kanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news