NA MWALIMU TUMAINI MASHINGO
NIKUMBUSHE awamu ambayo Simba na Yanga walifanikiwa kufanya makubwa kwenye mpira wa Afrika zaidi ya awamu ya sita (6) nipo pale nimeketi naomba useme bila kusita, nikumbushe awamu ambapo mpira ulipiga hatua na timu zikafanya makubwa kuliko awamu ya Sita, naweka roho sio pesa, mje Mpanda mnichukue mkanitupe daraja la Mkapa.

Samia binti Jangwani bado aliwaambia wazi GSM na wafanyabiashara kuwa hawabani bani kwenye kodi kwakuwa anataka kile kinachosalia wakakitumie haswa kwenye michezo, anataka Watanzania waneemeke na anataka klabu zetu zipige hatua, nikumbusheni lini Yanga alicheza fainali ya Shirikisho ama robo fainali ya Klabu bingwa, zaidi ya awamu ya sita.
Sasa nimehamia Mtaa wa pili napata kwanza supu ya Pweza na Mahindi ya kuchoma, nawasalimu watu wa bonde la Mto Msimbazi, nipo hapa kwa niaba ya Samia Bint Msimbazi ni Mzaliwa wa Unguja aliyeamua kuuishi Utamaduni wa Wauza simu na nguo, mitaa ya Ubize Msimbazi ilipo klabu ya Simba, mnasemaje mko fresh? Baada ya misimu mingi kuishia robo na sasa awamu ya Sita mpo Nusu fainali ya Shirikisho ni furaha iliyoje.
Samia Bint Msimbazi, Mwanamichezo nambari moja amemwaga fedha za kutosha kwenye goli la Mama, ameongeza mzigo kweenye mechi ya mwisho ya robo fainali kutoka Million tano mpaka million 10 kwa goli, ni mahaba yake kwa mchezo huu pendwa na timu zake, ni mahaba yake kutaka soka la Tanzania lipige hatua, Samia wa Kizimkazi ameipeleka Simba Nusu fainali na pasi na shaka anaiwaza fainali.
Nikumbushe lin na awamu ipi soka Ngazi ya Klabu nchini lilipiga hatua kubwa namna hii, nikumbushe lini soka la Tanzania limesumbua Afrika namna hii, Mama aliingia Simba ni ya 14 kwa ubora Afrika mpaka sasa Simba ni nafasi ya nne (4) kwa ubora barani Afrika, tumpe pongezi, tumsifu kwakuwa Yanga alikuwa nafasi ya 26 na sasa amesogea mpaka nafasi ya 11 Afrika, ni juhudu ya serikali yake sikivu, Mpenda Michezo na ndie Mwana Kariakoo namba moja.