DODOMA-Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mh. Emily Burns leo wamekutana jijini Dodoma na kufanya kikao juu ya maendeleo ya sekta ya madini nchini.

Aidha, Balozi Burns ameonesha utayari wa serikali ya Canada kutoa mafunzo maalum (Tailor- made training) kwa wakinamama na Vijana kupitia vyuo vya Ufundi-VETA katika maeneo ambapo uzalishaji madini unafanyika kwa wingi.
Balozi Burns ametumia pia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mageuzi makubwa yanayofanyika kwenye sekta ya madini hadi kupelekea kuongezeka kwa mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kufikia asilimia 10.1 kwa mwaka 2024.
Waziri Anthony Mavunde ameishukuru serikali ya Canada kwa dhamira yake ya kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza sekta ya madini huku msisitizo mkubwa akiuweka katika ushirikiano wa Utafiti wa Kina wa upatikanaji wa madini nchini ili kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi za uwingi wa madini nchini.
