Tanzania na Czech wajadili kusaini mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili

DODOMA-Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha, Bw. Meshack Anyingisye, kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu – El Maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Czech, uliongozwa na Balozi wa Czech nchini Kenya, Mhe. Nicol Adamcova, katika ofisi za Wizara ya Fedha jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine, yalilenga utiaji saini wa Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech ambao unatarajiwa kuweka mazingira ya kodi yanayotabirika ili kuvutia uwekezaji wa mitaji ya muda mrefu pamoja na kuondoa mzigo wa utozaji kodi mara mbili kwa wawekezaji wanaondesha shughuli zao kati ya nchi hizo mbili.

Kikao hicho kilimshirikisha Kamisha Msaidizi wa Sera, Wizara ya Fedha, anayeshughulikia masuala ya kodi za Kimataifa, Bw.Juma Mkabakuli.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Czech zilikamilisha majadiliano ya Mkataba wa Kuondoa Utozaji Kodi Mara Mbili mwaka 2024 na kwa sasa taratibu zote za kisheria za ndani kwa nchi zote mbili zimekamilika kwa ajili ya kusainiwa ili mkataba huo kuridhiwa na kuanza utekelezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news