DODOMA-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa muda wa siku sita kwa nchi za Afrika Kusini na Malawi kuondoa vikwazo vya kibiashara vinavyokwamisha wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kuuza mazao yao katika nchi hizo.

"Hakuna zabibu zozote wala apples pamoja na mazao mengine kutoka Malawi na Afrika Kusini yatakayoingia hapa nchini bila wao kuondoa vizuizi ili mazao ya Tanzania yaingie kuuzwa," amesema.
Ameongeza kuwa Tanzania haiwezi kuendelea kuwa muathirika wa vikwazo ambavyo haina hatia navyo, huku akisisitiza msimamo wa serikali:
"We are not losers kwenye hili game, kama hawaondoi, hakuna zao lolote la kwao litaingia hapa nchini. Niwaambie tu wafanyabiashara, kwenye hilo hakuna kitakachoendelea."
Bashe amefafanua kuwa serikali ya Tanzania haijawahi kuweka vizuizi kwa mazao kutoka nchi hizo kuingia nchini, hivyo haoni sababu ya wao kufanya hivyo kwa Tanzania:
"Haijawahi kutokea serikali kuzuia mazao yao kuingia hapa nchini. Sasa iweje wao wazuie mahindi kutoka Tanzania halafu wanyamaze? Kitu hicho hakiwezekani."
Amesisitiza kuwa hakuna madhara yatakayompata Mtanzania kutokana na kutoingia kwa baadhi ya bidhaa kutoka nje:
"Hakuna Mtanzania yoyote atakayepoteza maisha kwa ajili ya kukosa kula apple kutoka Afrika Kusini au zabibu za nchi hizo. Wataendelea kutumia mazao ya hapa nchini."
Ameeleza pia kuwa Tanzania imekuwa jirani mwema, ikisaidia hata wakati nchi hizo zina uhaba wa chakula, lakini sasa hali imebadilika:
"Nchi haijawahi kumsumbua jirani yoyote kwenye soko la mazao. Mara nyingi wakiwa na njaa wanapiga hodi na kusaidiwa. Sasa safari hii hakuna ndizi wala bidhaa yoyote ambayo itaingia hapa nchini."
Aidha, amewapa pole wafanyabiashara wa Tanzania waliopata usumbufu katika kuuza mazao yao nje, huku akiwahakikishia kwamba hatua madhubuti zimechukuliwa:
"Wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi wowote, kila kitu kita kaa sawa. Safari hii hakuna bidhaa yoyote ya kilimo ambayo itapokelewa kama nchi hizo hazitafungua mipaka hiyo.Wafanyabiashara wasibebe kitu chochote kutoka katika nchi hizo."