DAR-Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kinapenda kuwatangazia washiriki,wadau wa sekta ya habari na umma kwa ujumla kuhusu mabadiliko ya tarehe na mahali pa kufanyika kwa hafla ya utoaji wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Maendeleo-Samia Kalamu Awards 2025.
Hafla hiyo, ambayo awali ilikuwa imepangwa kufanyika tarehe 29 Aprili 2025 katikaUkumbi wa Mabele,Mabeyo Complex, jijini Dodoma, sasa itafanyika tarehe 5 Mei 2025 jijini Dar es Salaam katika ukumbi utakaotangazwa hivi karibuni.
Mabadiliko haya yanatokana na sababu za kiutendaji zisizoweza kuepukika.
Aidha, waalikwa wote watatumiwa mwaliko mpya wenye maelezo kamili kuhusu eneo na ratibaya tukio hilo.
Mgeni Rasmi katika tukio hili anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko haya na tunawashauri washiriki wote kuendelea na maandalizi ya kushiriki kwenye hafla hii adhimu inayolenga kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa wanahabari katika maendeleo ya taifa letu.
Tags
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Samia Kalamu Awards
TAMWA Tanzania