UWT Morogoro Mjini waamua tarehe nne kuyasema yote ya Rais Dkt.Samia

MOROGORO-Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Morogoro Mjini mkoani Morogoro umeandaa kongamano kubwa la kihistoria la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka minne ya dhahabu ya kazi zake zilizotukuka.
Hayo yamesemwa na Judith Joseph Laizer ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Morogoro Mjini mkoani Morogoro.

"Ninapenda kuwaalika wanawake wote wa Manispaa ya Morogoro Mjini na viunga vyake kwenye kongamano kubwa la kihistoria la kumpongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa miaka minne ya dhahabu ya kazi zake zilizotukuka."

Kwa nini wanawake wa Morogoro Mjini wameamua kufanya hivyo, Judith amesema, wameamua kufanya hivyo kwa sababu wanataka kuudhirishia umma kwamba Rais Samia ametekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo.

"Tumefanya hivi kuudhirishia umma kwamba Rais wetu kipenzi Mama Samia ametekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si kwa maneno."

Judith amesema, kongamano hilo watalifanya Aprili 4, 2025 kuanzia majira ya saa nne ambapo kongamano litatanguliwa na maandamano kutoka Ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro Mjini mpaka Ukumbi wa Mango ambapo ndipo shughuli yao itafanyika."

Judith ametoa wito kwa wanawake wote wakiwemo makada wote kushiriki katika kongamano hilo la kihistoria.

"Ni kongamano la kutaja na kuelezea miradi kabambe ambayo imetekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Daktari Samia Suluhu Hassan.

"Hii si ya kukosa, tutakuwa na watoa mada mbalimbali, lakini pia tutakuwa na vikundi mbalimbali vya kutumbuiza, wasanii wengi wa kike watakuwepo.

"Lakini, tutakuwa na ngoma pendwa ya asili, ngoma yetu ya Morogoro Mjini inayoitwa Kigoma cha Uruguai."

Judith amesema, wamedhamiria kufanya kongamano hilo kwa sababu Dunia nzima inajua mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt.Samia.

"Wanawake wa Morogoro Mjini tumeona kazi alizozifanya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa miaka minne ni nyingi kuliko kipindi alichokaa madarakani."

Amesema, wameona warudie kuueleza umma na Dunia nzima ijue mambo makubwa ambayo Rais Dkt.Samia ameyafanya.

"Tueleze kinagaubaga bila kufichana,tutakuwa na waandishi wa habari, vyombo vyote vitakuwepo, Dunia itazizima tarehe nne kwa ajili ya kusikiliza mambo makubwa, kazi kubwa zilizofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Kama amepokea pongezi nyingi kutoka mataifa ya nje na sisi tunaungana na wale wote waliotoa pongezi kwa sababu hazitoshi hizo pongezi, tumeamua kuunga nao na sisi kumpongeza Mheshimiwa Rais na kuwaeleza wananchi mambo makubwa ambayo Mama ameendelea kuyafanya ndani ya Taifa letu."

International news

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post