ROME-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ametembelea Ubalozi wa Tanzania mjini Rome nchini Italia akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo na kuzungumza na wafanyakazi wa Ubalozi huo ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha nchi kupitia diplomasia ya uchumi katika Taifa hilo baada ya kupokea taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Ubalozi huo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kituo cha Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Bi. Eva Kaluwa.