DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa usiku wa leo Aprili 5, 2025 anaongoza harambee ya kuwezesha maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo.