DAR-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imeendelea kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara (NBCPL) baada ya kufikisha alama 67.
Ongezeko la alama hizo linatokana na ushindi wa Aprili 10,2025 walioupata dhidi ya Azam FC katika Dimba la Azam Complex lililopo Chamanzi jijini Dar es Salaam.
Kwa sasa Yanga SC wamesogea mpaka alama 10 mbele ya Simba SC huku wakiwa wamecheza mechi 25.
Dube anaendelea kuwa kinara wa magoli kwenye ligi kuu mpaka sasa akiwa na magoli 12 sawa na Jean Charles Ahoua wa Simba SC.
Peodoh Pacôme Zouzoua dakika ya 12 ndiye aliayeanza kufungua pazia la mabao huku Prince Dube dakika ya 34 akiongeza bao la pili.
Mabao hayo yalidumu kipindi chote cha kwanza, ambapo kipindi cha pili Lusajo Elukaga Mwaikenda dakika ya 82 aliipa Azam FC bao la kufuta machozi.
Tazama msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Aprili 10,2025;